Tuesday, July 28, 2020

Mo Amtumia Rais Magufuli Ujumbe Mzito

DailynewsMfanyabiashara Mohammed Dewji ametuma ujumbe wa kumshukuru Rais John Magufuli kwa kukubali ombi la kubadilisha jina la uwanja wa taifa ulipo jijini Dar es salam kuitwa jina la Rais msataafu Benjamin Mkapa.

Dewji ambaye pia ni muwekezaji wa klabu ya Simba inayoshiriki ligi kuu bara amewashukuru pia watu ambao walijitoa kuunga mkono mawazo yake hayo ya kubadili jina la uwanja huo.

“Tunamshkuru Mh. Magufuli kwa kuridhia kubadili jina rasmi la Uwanja wa Taifa kuwa Uwanja wa Mkapa. Ahsante kwa wote tulivyo unganisha nguvu kufanikisha hilo. Kwa hakika tutaendelea kumuenzi na kuiletea heshima Tanzania kila mara tutakapo tumia Uwanja” amendika Mo Dewji.

Rais John Magufuli ametangaza leo kubadilia jina uwanja huo ulijengwa kwenye awamu ya tatu chini ya Rais Benjamin Mkapa aliyefariki dunia hivi karibuni.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/28/mo-amtumia-rais-magufuli-ujumbe-mzito/

No comments:

Post a Comment