Alimuua mwanawe baada ya kutofautiana na mumewe. Picha: Hisani
Mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Kipsagamu, eneo la Saboti Kaunti ya Tranzoia amewaacha wengi vinywa wazi baada ya kumuuua mwanawe wa miezi mitano na kumzika katika shamba la jirani yake.
Inadaiwa kuwa mwanamke huyo alichukua hatua hiyo ya kumuua mwanawe baada ya kujibizana na mumewe.
Kulingana na jirani huyo, aligundua shimbo isiyo ya kawaida katika shamba lake na hapo ndipo akamjuza mumewe. Mume huyo aliamua kuchimbua ili kuona kilichozikwa katika shimo hilo.
Alishangaa kupata mwili wa mtoto mdogo ukiwa umefungwa kwa taulo ndani ya shimo hilo.
Walitoka upesi na kusambaza ujumbe kwenye kijiji kuhusu mtoto aliyezikwa katika shamba lake.
Wanakiji walifika upesi kuona kisa hicho cha ajabu, babake mtoto huyo akiwa kati yao. Alichojua ni kuwa mkewewe alitotoka nyumbani akiwa na mtoto.
Baada ya mtoto huyo kufunuliwa, bwana huyo alipigwa na bumbuazi kugundua kuwa mwanawe ndiye aliyezikwa katika shamba hilo.
Kamanda wa polisi wa eneo hilo Ayub Gitonga alithibitisha kisa hicho na kuwashauri wanafamilia kusuluhisha tofauti zao bila kuhusisha vita na mauaji.
Haijabainika walichokuwa wakijibizania wawili hao na kupelekea kifo cha mtoto huyo.
Mwili wa mtoto huyo ulipekewa katika chumba cha kuhifadhia mati cha hospitali ya Kitale huku olisi wakianza msako mkali dhidi ya mama huyo aliyemuua mwanawe.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/27/mwanamke-amuua-mwanawe-wa-miezi-5-amzika-katika-shamba-la-jirani/
No comments:
Post a Comment