Msemaji mkuu wa serikali Dkt. Hassan Abbasi amesema baadhi ya viongozi wa mikoa na wilaya nchini wataanza kuaga mwili wa aliyekuwa rais wa Tanzania Benjamin Mkapa leo Julai 27, 2020 kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Akizungumza na wanahabari Dkt.Abbasi amesema sio kila kiongozi atapata nafasi ya kuaga mwili wa mzee Mkapa siku ya Jumanne kwenye shughuli ya kitaifa hivyo ni vyema wengine wakaanza kuaga leo ili kurahisisha zoezi hilo.
“Tumepokea salamu za rambi rambi kutoka nchi mbalimbali na bado tunaendelea kupokea salamu nyingi, baadhi ya viongozi na wawakilishi tumewasogeza waanze kuaga mwili kesho (Leo Julai 27, 2020) kurahisisha zoezi hilo kesho maan tutakuwa na wageni wengi”amesena Dkt Abbasi.
Aidha msemaji wa Serikali amewataka wananchi kendelea kujitomeza kwa wingi kwenye uwanja wa Uhuru kumuaga Rais huyo msaafu aliyefariki kutokana na mshtuko wa moyo.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/27/viongozi-wa-kiserikali-kumuaga-mkapa-leo/
No comments:
Post a Comment