Tuesday, July 28, 2020

Dondoo za leo: Jinsi familia ya Mkapa ilivyonusurukia kuuawa kwa tuhuma za uchawi, JPM asimulia alichoteta dakika za mwisho na Mkapa na Lissu asema ni vigumu kueleza hisia zake

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News ni siku nyingine ya Jumatatu Julai 27, 2020, matumaini yetu upo salama na karibu katika ujenzi wa taifa.

Tunakukaribusha katika dawati letu la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazopamba asubuhi ya leo.

Habari hizo ni jinsi familia ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa ilivyonusuruka kuuawa kwa tuhumu za uchuwi, JPM aanika walichoteta dakika za mwisho na Mkapa na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu asema ni vigumu kueleza hisia alizokuwa nazo aliporejea nyumbani.

Karibu msomaji wetu;

JINSI FAMILIA YA MKAPA ILIVYONUSURUKA KUUAWA KWA TUHUMA ZA UCHAWI

Katika maisha ya kimasikini kwenye kijiji cha Lupaso, familia ya hayati Benjamin Mkapa ilikuwa inaonekana kuwa na maisha mazuri.

Utofauti wa familia hiyo na wengi kijini hapo ulitokana na uhakika wa kipato alichokuwa akikipata kila mwisho wa mwezi. Hilo halikuwafurahisha wengi na kujenga wivu uliosabisha kutokea kwa shambulio ambalo nusura liangamize familia yao.

Hicho ni moja ya visa vya maisha ya hayati rais mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania ambacho amekihadithia mwenyewe katika kitabu chake cha maisha yake ambacho alikizindua Disemba 2019. Mzee Mkapa alifariki usiku wa kuamkia Ijumaa na anazikwa leo kijijini Lupaso kusini mwa Tanzania.

Baba yake, William Matwani alikuwa Katekista wa Kanisa Katoliki kijijini hapo pamoja na kufanya kazi ya ualimu, hivyo alikuwa na kipato cha uhakika, kila mwisho wa mwezi, japo kilikuwa kidogo, lakini halikuwa jambo la kawaida katika kipindi hiko cha ukoloni.

“Jambo jengine ambalo ni la nadra ni kuwa watoto wote wanne katika familia yetu, pamoja na dada yangu, tulikuwa tumesoma. Hii ilimaanisha kuwa tulikuwa na mustakabali mzuri maishani lakini pia ilitutofautisha na wengine kijini kwetu,” hayati Mkapa anasimulia katika kitabu chake.

Soma zaidi

JPM AANIKA WALICHOTETA DAKIKA ZA MWISHO NA MKAPA

 

RAIS John Magufuli ameeleza alivyozungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, na kumpa maneno ya mwisho saa chache kabla ya kifo chake.

Mkapa (1938-2020), alifariki dunia usiku wa kuamkia Ijumaa hospitalini jijini Dar es Salaam kutokana na shambulio la moyo.

Katika hotuba yake jana wakati wa kuaga mwili wa Mkapa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini na baadaye kusafirishwa kwenda kijijini kwake Lupaso wilayani Masasi mkoani Mtwara kwa mazishi yatakayofanyika leo mchana, Rais Magufuli alifunguka walichoteta na kiongozi huyo.

Rais Magufuli alisema alipata fursa ya kuzungumza naye saa chache kabla ya umauti kumfika, akisema: “Binafsi nilipata fursa ya kuongea na Mzee Mkapa kwa njia ya simu akiwa hospitalini saa chache kabla hajafariki (dunia).

Soma zaidi

LISSU: NI VIGUMU KUELEZEA HISIA NILIZOKUWA NAZO NILIPOREJEA NYUMBANI

Ni siku mbili baada ya kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu kuwasili nchini mwake akitokea Ubelgji kwa matibabu baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana amezungumza na BBC.

Katika mahojiano haya na Mwandishi Scolar Kisanga Lissu anaelezea hisia zake kuhusu mapokesi aliyoyapata, fursa yake katika uchaguzi wa urais wa mwezi Oktoba na suala la yeye na wanachama wenzake wa CHADEMA kutoruhusiwa kuingia katika shughuli ya kuuaga mwili wa Hayati rais wa awamu ya tatu wa Tanzania Benjamin William Mkapa aliyefariki dunia.

Soma zaidi



source http://www.bongoleo.com/2020/07/29/dondoo-za-leo-jinsi-familia-ya-mkapa-ilivyonusurukia-kuuawa-kwa-tuhuma-za-uchawi-jpm-asimulia-alichoteta-dakika-za-mwisho-na-mkapa-na-lissu-asema-ni-vigumu-kueleza-hisia-zake/

No comments:

Post a Comment