Wednesday, July 29, 2020

Hatimaye Mkapa Apumzishwa Lupaso

ImageBaada ya kufariki Dunia usiku wa kuamkia Julai 24, 2020 hatimaye leo mwendazake Rais mstaafu Benjamin Mkapa amepumzishwa kwenye nyumba yake ya milele kwenye eneo alilochagua mwenyewe kipindi cha uhai wake kijijini  Lupaso, wilayani  Masasi mkoani Mtwara.

Shughuli hiyo ambayo imeongozwa na Rais John Magufuli imehuzuliwa na mamia ya wakazi wa Lupaso pamoja na viongozi wa kiserikali na mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.

Mkapa ambaye aliongoza Tanzania kwanzia mwaka 1995 hadi 2005 alifariki baada ya kulazwa kwa siku kadhaa kwenye hospitali moja jijini Dar es salaam akisumbuliwa na ugonjwa na malairia alifariki baada ya kupata mshtuko wa moyo akiwa bado anapatiwa matibabu usiku wa Julai 23, 2020.

Mkapa ameacha mjane na watoto wawili pamoja na wajukuu kadhaa, enzi za uhai wake Mpaka alijizolea umaarufu kote dunia kutokana na kutatua migogoro mbalimbali ya kisiasa kwenye nchi za afrika mashariki na kati.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/29/hatimaye-mkapa-apumzishwa-lupaso/

No comments:

Post a Comment