Wednesday, July 29, 2020

Mwijaku Afikishwa Mahakamani Kisa Picha Za Utupu

ImageMsanii wa Filamu nchini, Brighton Mwemba maarufu kama Mwijaku amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka moja la kusambaza picha za utupu kinyume cha sheria.

Mwijaku ambaye alikuwa mmoja kati  ya watia nia wa ubunge kwenye jimbo la Kawe kupitia chama cha mapinduzi (CCM) amefikishwa mahakakani hapo leo Julai 29, 2020.

Mwijaku anadaiwa kuchapisha picha hizo Septemba 15 na Oktoba 10 mwaka 2019 kwa kutumia mfumo wa kompyuta kupitia mtandao wa WhatsApp.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/29/mwijaku-afikishwa-mahakamani-kisa-picha-za-utupu/

No comments:

Post a Comment