Rais John Pombe Magufuli aliwaongoza waombolezaji katika hafla ya mazishi ya Mzee Benjamin Mkapa
Alimtaja Mkapa kama mshauri wa ajabu na kiongozi wa kuigwa
Alieleza kuwa atataka kuzikwa katika kijiji chao sawa na alivyoagiza Mkapa akiwa hai
Serikali ilitenga sehemu maalum kuwazika vingozi wakuu wa Tanzania Dodoma
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania DKt John Pombe Magufuli aliwaongoza Watanzania pamoja na viongozi wa tabaka mbali mbali katika hafla ya mazishi ya hayati aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa.
Magufuli alimrundia sifa sufufu hayati akimtaja kama mshauri wa aina yake na kiongozi wa kuigwa.
Safari ya mwisho ya Mzee Mkapa. Picha: Hisani
Si hilo tu, Rais Pombe alieleza kuwa yuko tayari kumuiga Mzee Mkapa hata kuhusu eneo maziko. Licha ya kuwepo eneo maalum iliyotengwa na serikali kuwazika viongozi, Mzee Mkapa alichagua kuzikwa katika kijiji chake cha Lupaso, Mtwara.
Magufuli naye alisisitiza kuwa wakati wake ufikapo, atataka kuzikwa katika kijiji chake
‘’Tulipangiwa kuzikwa Dodoma maana ndiyo makao makuu, miaka miwili mitatu, Mzee Mkapa akaniuliza, mlipanga maziko yaye Dodoma? Mimi mnizike Lupaso, nikamuuliza Kikwete,… mimi Lusoga…Kwenye dhamiri yangu na mimi nitazikwa Chato.’’ Alisema Rais Magufuli.
Aidha, Rais huyo alieleza kuwa aliamua kulirudisha ardhi iliyyotengewa mazishi ya viongozi kwa wenyeji wa Dodoma ili kutumika kwa shughuli za maendeleo.
Magufuli aliwakumbusha Watanzania na waombolezaji kwa jumla kuhusu swala la kila mtu kupenda kwao kama alivyofanya Mzee Mkapa.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/29/rais-magufuli-afichua-atakapozikwa-siku-yake-ifikapo/
No comments:
Post a Comment