Saturday, July 25, 2020

Rais Dk. Shein asema Mkapa amesaidia kuibadilisha nchi

Rais wa Zanzibar, Dk. Mohamed Shein amesema Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa amesaidia kuibadilisha nchi.

Amesema amefanya mabadiliko ya kiuchumi, ameanzisha suala zima la utawala bora.

“Si nchi nyingi za Afrika zina utawala bora, yeye kaanzisha wizara ya mwanzo ya utawala bora hapa Afrika amesimamia kwa vitendo sio kwa maneno,” alisema.

Aliongezea kuwa “Nimefanya nae kazi nikiwa Makamu wa Rais, alipenda sana amani ya nchi yetu na maendeleo ya nchi, hakika tumeondokewa ni msiba mzito ndani na nje ya nchi, kubwa ni kumuombea apumzike salama,”

Rais Mkapa amefariki usiku wa kuamkia jana  akiwa amelazwa hospitali jijini Dar es Salaam.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/25/rais-dk-shein-asema-mkapa-amesaidia-kuibadilisha-nchi/

No comments:

Post a Comment