Aliyekuwa mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA) Joseph Mbilinyi amesema yajayo baada ya kumpokea makamu mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu aliyerejea nchini leo Julai 27, 2020 baada ya miaka mitatu yanafurahisha.
Mbilinyi alikuwa mmoja kati ya mamia ya wananchadema waliojitokeza kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere kumpokea Lissu.
“Tumeshampokea SHUJAA…Hakika yajayo sasa lazima YATAFURAHISHA…” ameandika Mbilinyi kwenye ukurasa wake wa Twitter na hukua ambatanisha video ya wanachadema waliojutokeza kumpokea Lissu.
Tundu Lissu anareje nchini ikiwa ni baada ya miaka mitatu ya kupatiwa matubabu nchini Ubeligiji baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana.
Tumeshampokea SHUJAA…Hakika yajayo sasa lazima YATAFURAHISHA… pic.twitter.com/7Tc8OANHly
— Joseph Mbilinyi (@IamJongwe__) July 27, 2020
source http://www.bongoleo.com/2020/07/27/ujumbe-wa-sugu-baada-ya-lissu-kutua-nchini/
No comments:
Post a Comment