Klabu ya Yanga imetangaza kuachana na aliyekuwa kocha wao Luc Eymael kutoka na kutoa kauli za kibaguzi kwa mashabiki wa soka nchini baada ya mchezo wa mwisho wa ligi kuu bara dhidi ya Lipuli FC jana.
Yanga imetoa taarifa ya kuacha na kocha huyo leo Julai 27, 2020 na kumtaka kuondoka nchini hapa haraka iwezekanavyo kutokana na kitendo alichokifanya hapo.
“Uongozi unawaomba radhi Viongozi wa nchi, Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa Yanga, pamoja na wananchi kwa ujumla kutokana na kauli za kuudhi na kudhalilisha zilizotolewa na Kocha Luc Eymael” imenukuliwa taarifa ya Yanga.
Luc alisikia jana akitoa kauli za kibaguzi kwa kudai mashabiki wa soka nchin hawaju ia mpira na wanapiga kelele bila kujua mbinu zozote za soka na mpira wa tanznaia hauwezi kuendelea hata kifog kutokana na tabaia ya mashabiki hao.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/27/yanga-yamtupia-virago-kocha-wake/
No comments:
Post a Comment