Korea Kaskazini haijaripoti kisa hata kimoja cha maambukizi ya covid19 miezi saba baada ya kulipuka virusi hivyo Uchina
Anayeshukiwa kuwa na dalili za virusi hivyo aliingia nchini humo Kinyume cha sheria Julai, 19 2020
Kiongozi wa Korea Kusini Kim Jong-un amechukua hatua ya kutangaza hali ya taharuki nchini humo baada ya madaktari wake kumtambua jamaa anayeshukiwa kuambukizwa virusi vya corona.
Iwapo mgonjwa huyo atapatikana na virusi vya corona, atakuwa wa kwanza kabisa kuambukizwa virusi hivyo hatari nchini humo.
Kwa mujibu wa idhaa ya taifa hilo KCNA, jamaa anayeonyesha dalili za virusi hivyo aliwasali nchini humo Jumapili, Julai 19 kutoka Korea Kaskazini alikokuwa kwa miaka mitatu.
Korea kaskazini lipiga marufuku utalii. Picha: Hisani
‘’ Hali ya taharuki ilitokea katika mji wa Kaesong ambapo jamaa aliyetorokea Korea Kusini miaka mitatu iliyopita alirudi nchini Julai 19 kinyume cha sheria akishukiwa kuwa na virusi vya corona,’’ taarifa ya KCNA.
Licha ya nchi hiyo kusisitiza kwa haina visa vyovyote vya maambukizi ya Covi19, baadhi ya mashirika ya uangalizi yamesisitiza kuwa hiyo siyo hali halisi.
Yameeleza kuwa Korea Kaskazini ni majarani ya Uchina na kulingana na mipaka hafifu kati ya nchi hizo mbili, kuna uwezekano mkubwa kuwa virusi hivyo vilishaingia nchini humo.
Kim Jong alichukua hatua ya kufunga mipaka yake Januari, 2020 baada ya maambukizi ya virusi hivyo kuripotiwa Uchina.
Hadi Jumapili, Julai 26, Korea kusini ambayo inapakana na nchi ya Jong ilikuwa imerokodi visa 14,150 ya maambukizi.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/27/korea-kaskazini-yatangaza-hali-ya-taharuki-kisa-cha-kwanza-cha-covid19-chashukiwa/
No comments:
Post a Comment