Friday, July 31, 2020

Takukuru inamshikilia mfanyabiashara Alute kwa kufanya utapeli wa nyumba na viwanja

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Manyara inamshikilia Japhet Samweli Alute kwa kufanya biashara ya mikopo umiza inayoambatana na kukopesha wananchi kwa ribs kubwa na kisha kuwadhulumu mali zao wanazo weka kama dhamana.

Alute anafanya biashara hiyo bima kuwa na leseni ya biashara, jambo ambalo linaikosesha serikali mapato kutokana na ukwepaji kodi.

Biashara ya fedha inatakiwa kupatiwa kibali cha Benki Kuu (BoT) jambo ambalo hakulitekeleza na hana leseni ya biashara.

Alute anatumia jina la Halmashauri ya mji wa Babati kuwatishia wananchi wanaochelewesha kufanya marejesho kwa kuwatumia ujumbe wa kuwauzia maeneo yao au nyumba walizoweka kama dhamana kwa mikopo umiza.

Mtuhumiwa huyo amepekuliwa na kupatikana na mikataba ya kitapeli 99 ambayo inaonyesha ameuza maeneo mbalimbali zikiwemo nyumba na viwanja vya wananchi Babati.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/31/takukuru-inamshikilia-mfanyabiashara-alute-kwa-kufanya-utapeli-wa-nyumba-na-viwanja/

No comments:

Post a Comment