Sunday, July 26, 2020

Mo amuomba Rais Magufuli kubadili jina la uwanja wa Taifa

Mfanyabiashara, Mohammed Dewji, maarufu kwa jina la MO amemuomba Rais John Magufuli kubadili jina la uwanja wa Taifa.

“Leo nimeamua kuanzisha petition (maombi) kwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kubadili jina la uwanja wa Taifa kuwa: Uwanja wa Benjamini William Mkapa,” aliandika MO katika ukurasa wake wa Twitter.

Dewji amesema itapendeza kama uwanja utaitwa jina la Uwanja wa Benjamin William Mkapa.

“Tunamuomba Rais John Pombe Magufuli aridhie kubadili jina la uwanja huo kwa heshima ya hayati Mkapa ili tuendelee kumkumbuka kwa mchango wake mkubwa hasa kwa vizazi vijavyo,”

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/26/mo-amuomba-rais-magufuli-kubadili-jina-la-uwanja-wa-taifa/

No comments:

Post a Comment