Tuesday, July 28, 2020

Lema Ashtuka Ukimya Wa Jeshi La Polisi Mapokezi Ya Lissu

Godbless Lema Arudishwa Tena Gerezani.....Ni Baada ya Serikali ...Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Godbless Lema ameonya wanachama na wapenzi wa chama hicho juu ya ukimya ulionyeshwa na jeshi la polisi jana wakati wa mapokezi ya makamu wa mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu alipowasilia nchini.

Lema ameonya hayo kupitia ujumbe alituma kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter amesema wapinzani wanapaswa kujiuliza maswali mengi na majibu yawe tofauti na fikra za watu wakawaida.

“Sina amani kwa tabia nzuri walioonyesha Jeshi la Polisi jana wakat wa mapokezi ya Mh Tundu Lissu. Nina paswa kujiuliza maswali mengi na majibu yawe tofauti na fikra za watu wengi, ninaona ni kama chloroquine imepakwa sukari,kuna kitu kina fikiriwa na sisi tuna paswa kufikiri zaidi” ameandika Lema.

Hapo jana Julai 27, 2020 mamia ya wanachama wa chama  hicho wamejitokeza kwa wingi kumraki makamu mwenyekiti wao Tundu Lissu aliyerejea nchini baada ya miaka mitatu ya kupatiwa matibabu nchini Ubeligiji.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/28/lema-ashtuka-ukimya-wa-jeshi-la-polisi-mapokezi-ya-lissu/

No comments:

Post a Comment