Ilikuwa furaha isiyo na kifani katika hospitali ya rufaa ya Kisii baada ya mgonjwa aliyekuwa akipata matiba hospitalini humo kufuatia maambukizi ya virusi vya corona kujifungua akiwa ametiwa kwenye ICU.
Mgonjwa huyo ambaye pia hufanya kazi kama muuguzi katika kaunti ya Homabay alijifungua mtoto wa kiume Ijumaa, Julai 24.
Kwa mujibu wa jarida la Standard, muuguzi huyo mwenye umri wa miaka 32 aliweka saini kuruhusi kufanyiwa upasuaji kama njia ya kumzalisha licha ya kujifungua kawaida usiku wa Ijumaa.
Mumewe mama huyo aliruhusiwa kumuona mkewe na mtoto waliotiwa katika karantini chini ya ungalizi mkali kulingana na kanuzi zilizowekwe na wizara ya afya.
‘’Nilingia na daktari nikiwa nimevalia magwanda ya kujikinga, nilimuona mtoto wangu akiwa kwenye kiangulio.’’
Kama haingekuwa mambo ya covid19, ningekuwa na mtoto wangu pamoja na mamake, ningekuwa nambeba mtoto. Ni vigumu lakini nawashukuru madaktari pamoja na hospitali kwa kazi waliyoifanya,’’ Mumewe alisema.
Bwana huyo ambaye pia alipimwa virusi vya corona bila kupatikana nayo alieleza kuwa walifanya harusi na mkewe mapema 2019.
Hangeweza kuficha furaha yake hata baada ya kueleza kuhusu jinsi alivyokuwa na hofu baada ya mkewe kuambikizwa virusi vya corona na kutiwa kwenye ICU.
Kulingana na bosi wa hospitali hiyo Enock Ondari, muuguzi huyo aliletwa hospitalini humo kutoka hospitali ya wilaya ya Rachuonyo baada ya hali yake kuzidi.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/27/mgonjwa-apatikana-na-covid19-ajifungua-akiwa-icu/
No comments:
Post a Comment