Jeshi la Polisi Nchini limetoa onyo kali kwa viongozi wanaohamasisha mikusanyiko ya watu isiyo zingatia sheria za nchi na yenye lengo ovu kwa taifa.
Kauli hii imetolewa leo Julai 25, 2020 kufuatia kuwepo kwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA wanaohamasisha watu kupitia mitandao ya kijamii kukusanyika kwenda kumpokea mmoja wa wanachama wao anayetarajia kuwasili nchini Tanzania kwenye uwanaja wa Mwalimu Nyerere Julai 27, 2020.
Jeshi la polisi limesema linatambua watanzani wapo kwenye kipindi cha maombolezo lakini hilo halitawazuia kuwawajibisha kwa mujibu wa sheria wale wote wanaokusudia kufanya mikusanyiko bila kuzingatia sheria.
Ameeleza kuwa jeshi la polisi lefuatilia nchi nzima kuona kama kuna taarifa iliyofikishwa kituo chochote cha polisi kwa ajili ya kusanyiko hilo wanaloliitisha katika muda uliotolewa kisheria lakini hakuna.
“Kukusanyika ni haki ya Mtanzania lakini hakuna haki isiyokuwa na wajibu kwa mujibu wa sheria za nchi,” taarifa hiyo ilieleza.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/25/jeshi-la-polisi-limetoa-onyo-kwa-chadema-kukusanyika-kwa-ajili-ya-mapokezi-ya-lissu/
No comments:
Post a Comment