Kiongozi was Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema ameshiriki mazishi Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kijijini kwake Lupaso mkoani Mtwara hakutumia nafasi yake kupendelea Wilaya yake kimaendeleo.
“Kuna mamjo kadhaa ambayo binafsi sikukubaliana na Rais Mkapa lakini kama ilivyo kwa Nyerere, Mwinyi na Kikwete hakutumia nafasi yake kupendelea Wilaya yake kimaendeleo,” aliandika Zitto.
Zitto aliandika ujumbe huo Jana katika ukurasa wake was twitter kuwa “Lupaso hakuna hifadhi ya taifa, hakuna uwanja wa ndege, sio wa kimataifa Bali hats airstrip, hakuna hospitali ya rufaa hakuna ofisi ya TRA, Zimamoto, wala Takukuru,”
Zitto amesema mawaziri wa Mkapa hawakukimbizana kumfurahisha kwa kupeleka miradi Lupaso.
Lupaso hakuna Hifadhi ya Taifa, hakuna Uwanja wa Ndege, sio wa kimataifa bali hata airstrip, hakuna Hospitali ya Rufaa, hakuna Ofisi ya TRA, Zimamoto wala TAKUKURU. Mawaziri wa Mkapa hawakukimbizana kumfurahisha kwa kupeleka Miradi Lupaso. Sikusikia mpango wa Chuo Kikuu Lupaso
— Zitto MwamiRuyagwa Kabwe (@zittokabwe) July 29, 2020
source http://www.bongoleo.com/2020/07/30/zitto-mkapa-hakutumia-nafasi-yake-kupendelea-maendelea-katika-wilaya-yake-ya-lupaso/
No comments:
Post a Comment