Friday, July 24, 2020

Msemaji wa Serikali Kenya Aambukizwa Covid19

Government spokesman Cyrus Oguna test COVID19 positive - WikiZiki.Com

Msemaji wa serikali Cyrus Oguna amepatikana na virusi vya corona. Picha: Hisani.

Oguna alithibitisha Ijumaa, Julai 24 kuhusu kuambukizwa virusi hivyo

Uvumi kuhusu kuambukizwa kwake  virusi vya corona ulienea wiki moja awali, uvumu alioukana vikali

‘’ Tumepokea ripoti inayosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa nimelazwa hspitalini. Nimewasili kutoka kazi nje ya jiji,’’ aliandika.

Huku uvumi ukienea kuwa baadhi ya mawaziri na viongozi wakuu serikali wamembukizwa virusi vya corona, msemaji wa serikali Cyrus Oguna amejitokeza na kutangaza bayana kuwa anaugua virusi hivyo.

Kupitia katika ukurasa wake wa Twitter, Oguna alithibitisha kuwa alikuwa akiugua virusi hivyo, na kuwa alikuwa amelazwa tayari karantini anakopata matibabu.

‘’ Nilikuwa na dalili za corona baada ya kurudi kutoka nje ya jiji la Nairobi kazini na nikafanyiwa vipimo.

Matokeo yalionyesha nina virusi hivyo na sasa napokea matibabu na kupata nafuu katika karantini,’’ alisema.

Maafisa katika wizara ya afya wanaopambana na virusi vya corona sasa wameanza oparesheni ya kuwatafuta watu walitamgamana na msemaji huyo wa serikali ili kutiwa karantini kama njia ya kuzui kusambaa kwa virusi hivyo.

Haya yanajiri siku mbili tu baada ya mwanahabari maarufu Jeff Koinange kujitokeza bayana kukiri kuwa aliambukiwa virusi hivyo licha ya kutokuwa na dalili zozote.

Wizara ya afya imewashukuru waliojitokeza kutangaza hali yao, ikiitaja kama njia bora ya kuihamasisha jamii.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/24/msemaji-wa-serikali-kenya-aambukizwa-covid19/

No comments:

Post a Comment