Monday, July 27, 2020

Kioja, Mama Amnasa Bintiye Ana kwa Ana na Mzee wa Miaka 57 Katika Tendo la Ndoa

Mama huyu alimpata mwanawe wa miaka 22 na mzee wa miaka 57 nyumbani kwake

Alitishia kulichoma gari la sugar daddy huyo walipokataa kufungua mlango

Alieleza kuwa mwanawe hana adabu na amemfanya awe na msongo wa moyo kwa muda

Ilikuwa sinema ya bure katika mtaa wa Zimmerman Nairobi baada ya mama kumnasa mwanawe wa kike mwenye umri wa miaka 22 wakilambishana asali kwenye nyumba yake na mzee wa miaka 57.

Mama huyo alifika kutoka kazini kama kawaida na kushangzwa na gari moja la kifahari nje ya nyumba yake, kilichomshangaza zaidi ni pale alipopata mlango umefungwa na sauti zisizoza za kawaida zikisikika ndani.

Mama huyo alibisha mara kadhaa bila kufunguliwa mlango, na ndipo akashuku na kuanza kupiga kamsa akisema analichoma gari hilo.

Mzee huyu aliposikia kuwa gari lake litateketezwa, alimsihi mwanadada huyo kufungua mlango.

Mama huyo alipigwa na bumbuazi kugundua kuwa mwanawe alikuwa akihusika katika tendo la ndoa na mzee rika ya babu yakekatika nyumba yake.

Majirani waliofika eneo hilo upesi walimuokoa jamaa huyo mikononi mwa umma wenye mori uliokuwa na nia ya kuliteketeza gari lake na kumpiga.

62 Stress Management Techniques, Strategies & Activities

Mama huyo alijawa msongo wa moyo. Picha; Hisani

Mama huyo alisimualia kuhusu jinsi mwanawe huyo ambaye ni mwanfunzi wa mwaka wa pili katika chuo kikuu amemkosesha usingizi kwa tabia zake mbovu.

Alieleza kuwa amefanya kila awezalo kuwatunza na kuwalea ipasavyo wanawe wawili wawili wa kike lakini wote wamekuwa aibu mtupu.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/28/kioja-mama-amnasa-mwanawe-ana-kwa-ana-na-mzee-wa-miaka-57-katika-tendo-la-ndoa/

No comments:

Post a Comment