Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imesema wameondoa sokoni kondomu feki 17,076 ambazo zimebainika zipi chini ya ubora unaotakiwa.
Kadhalika, sababu ya kuadimika kwa bidhaa hiyo imetajwa ni kutokana na kubaini hazipo katika ubora unaotakiwa na kuzuiliwa kuingia sokoni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Kaimu Mkurugenzi wa Dawa na Vifaa Tiba wa TMDA, Akida Khea, katika kikao kazi cha waandishi wa habari wa mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro kinachohusu usimamizi wa sheria ya dawa na vifaa tiba sura ya 19.
Khea amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2019/20 ndipo wamebaini idadi hizo feki za kondomu na kuzuia zisiingizwe sokoni.
Amezitaja aina ya Kondomu hizo ni Life Guard, Ultimate, Maximum Classic, Pudence na Chishango.
Aidha, amesema wamekuwa wakizuia bidhaa zinazoingia sokoni ambazo hazijakidhi vigezo vya ubora unaotakiwa.
Amesema huwa bidhaa hizo wanazifanyia uchunguzi kabla hazijamfikia mteja.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/28/kondomu-feki-17076-zimeondolewa-sokoni/
No comments:
Post a Comment