Sunday, July 26, 2020

Dondoo za leo: Kilichosababisha kifo cha Mkapa, Sumaye asema alimkatalia Mkapa kuwa Waziri Mkuu na Lissu kurejea leo aweka video akiwa uwanja wa ndege na viongozi

 

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News ni siku nyingine ya Jumatatu Julai 27, 2020, matumaini yetu upo salama na karibu katika ujenzi wa taifa.

Tunakukaribusha katika dawati letu la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazopamba asubuhi ya leo.

Habari hizo ni je unajua kilichosababisha kifo cha Rais Mstaafu Benjamin Mkapa?, Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye asimulia jinsi alivyomkatalia Rais Mstaafu Mkapa kuwa Waziri Mkuu kulikoni alitaka kukataa? na Lissu kuingia leo mchana atuma video akiwa anaelekea kupanda ndege jana usiku.

Karibu msomaji wetu

KILICHOSABABISHA KIFO CHA MKAPA

FAMILIA ya Rais mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu, Hayati Mzee Benjamin Mkapa (81), imeeleza sababu za kifo chake kuwa ni mshtuko wa moyo.

Familia ilieleza jana katika ufafanuzi wake kuwa Mzee Mkapa alipata mshtuko wa moyo baada ya kuugua malaria kwa siku mbili na kulazwa hospitalini.

Msemaji wa Familia, William Erio, akitoa taarifa wakati wa Misa Takatifu ya kuaaga mwili wa Mzee Mkapa, alisema kumekuwa na uzushi mwingi kwenye mitandao ya kijamii, na kwamba ukweli ni kuwa alipata mshtuko wa moyo akiwa amekaa.

“Sababu ya kifo chake ni mshtuko wa moyo…nilidhani ni vizuri tuliseme maana kumeanza kuwa na maneno na maelezo ya kila mtu akijifanya ni mwelewa, nabii katika mitandao ya kijamii na katika sehemu nyingine,” alisema Erio na kuongeza:

Soma zaidi

SUMAYE: NILIMKATALIA MKAPA UWAZIRI MKUU

 

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amesema alikuwa mtu mwenye bahati kufanya kazi chini ya uongozi wa Benjamin Mkapa kama msaidizi wake katika uwaziri mkuu ingawa alikataa cheo hicho hapo awali alipoitwa naye Ikulu na kupewa taarifa hiyo.

“Nimefanya naye kazi kwa miaka 10 kama waziri wake, lakini kabla ya hapo nilifanya naye kazi katika serikali nikiwa Naibu Waziri naye akiwa Waziri katika wizara tofauti.

Kipindi hicho sikuwa karibu naye hadi aliponichagua kuwa Waziri Mkuu wake wakati huo akiwa rais, “Baada ya uchaguzi mwaka 1995, saa 8:00 mchana aliniita Ikulu, wakati huo Bunge lilikuwa linajiandaa kwenda kikaoni kupokea jina la Waziri Mkuu na kuniambia mimi ndiye Waziri Mkuu, nilimwomba anibadilishe nafasi hiyo alikataa na kwa kuwa sikuwa na mamlaka ya kupinga kauli yake, ilinibidi nikubali,” alisema Sumaye katika mahojiano na Tv jana.

Alisema alipotoka Ikulu na kwenda nyumbani kwake, alimfahamaisha mkewe kuhusu uteuzi huo ambaye kama ilivyokuwa kwake alihoji kama amekubali kupewa cheo hicho ambapo alimueleza hata yeye alikataa ila ilimlazimu.

Soma zaidi

LISSU ATUPIA VIDEO AKIWA ANAENDA KUPANDA NDEGE

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, ameonyesha picha ya video wakati akiende kupanda ndege.

Katika video hiyo Lissu aliongozana na mkewe, dereva wake wakiwa wanatembea kuelekea uwanja wa ndege kwa ajili ya kuanza safari jana usiku kuja Tanzania.

Soma zaidi

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/27/dondoo-za-leo-kilichosababisha-kifo-cha-mkapa-sumaye-asema-alimkatalia-mkapa-kuwa-waziri-mkuu-na-lissu-kurejea-leo-aweka-video-akiwa-uwanja-wa-ndege-na-viongozi/

No comments:

Post a Comment