Friday, July 31, 2020

Tanzania yaifungia Kenya kuleta ndege zake nchini

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imefuta kibai kilichokuwa kinarusha ndege za Shirika la Ndege la Kenya (KQ) kutua Tanzania.

Uamuzi huo umekuja baada ya Kenya kutoiweka Tanzania katika orodha ya nchi ambazo raia wake wataruhusiwa kuingia Kenya kuanzia Agosti 01, 2020.

Kwa mujibu wa taarifa iiyotowa jana kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari, ameeeza Kenya wametangaza kuwa Agosti 01, 2020 kufungua anga lake kwa usafiri wa  ndege za kimataifa kuanza kuingia nchini Kenya tangu walivyozuia Marchi 25, 2020.

Hamza Johari

Taarifa hiyo imeeleza kuwa ndege ya Kenya (KQ) inayofanya safari zake  Dar es Saaam, Kilimanjaro na Zanzibar hazitakiwi kuingia Tanzania kutokana na notisi waliyoitoa mpaka watakapotangaza tena.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/01/tanzania-yaifungia-kenya-kuleta-ndege-zake-nchini/

No comments:

Post a Comment