Wednesday, July 29, 2020

Rais Magufuli asimulia sababu ya Mkapa kuchagua kuzikwa kijijini kwake Luupaso

 

Rais John Magufuli amesema Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa alichagua eneo la kuzikwa liwe kijijini kwake Lupaso na sio mkoani Dodoma.

“Tulipangiwa viongozi kuzikwa Dodoma , Mzee Mkapa akaniuliza mlipanga maziko yawe Dodoma nikasema wewe unataka wakuzike wapi akasema Lusapo, Mzee Kikwete akasemaMsoga nikaogopa kumuuliza Mzee Mwinyi lisije kutokea lolote nikaonekana nimemchuria na mimi nilisema nitazikwa Chato,” amesema Magufuli

“Nikaona hilo eneo labda atazikwa mzee Malecella kwa sababu kwao ni Dodoma na kwa vile hatalitumia lote lile eneo nikawarudishia wananchi wa Dodoma kwa sababu hakuna hata mmoja anayetaka kuzikwa Dodoma kila mmoja anataka azikwe kwao na aliyeanzisha huu utaratibu ni mzee Mkapa kwa hiyo Mkapa alipenda kwao kwenye hili nafikiti Watanzania trunashukuru Mzee Mkapa angeweze kuchagua Dar es Salaam kwa kuwa ana eneo kubwa lakini ndani ya dhamira yake alitaka azikwe kwenye kijiji alichozaliwa Lupaso,” amesema Magufuli.

Aidha, Magufuli amesema Mkapa ni mtu ambaye ni mzalendo na aliipenda nchi yake kwa kuonyesha upendo wa kweli.

“Sina mengi zaidi tuendelee kumuombea mama Mkapa pamoja na familia waendelee kuishi kwa upendo na kumtanguliza Mungu,” amesema Magufuli.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/29/rais-magufuli-asimulia-sababu-ya-mkapa-kuchagua-kuzikwa-kijijini-kwake-luupaso/

No comments:

Post a Comment