Wednesday, July 29, 2020

Ibada ya mazishi ya Rais Mstaafu Mkapa ikiendelea, watu wafurika kumuaga

Ibada ya mazishi ya Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa, bado inaendelea katika kijiji cha Lupaso mkoani Mtwara.

Viongozi mbalimbali  akiwemo Rais John Magufuli, Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Waziri Mkuu, Kassim Mjalaliwa, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Spika wa Bunge, Job Ndugai walishirika ibada hiyo.

Wapo viongozi wengine mbalimbali wa ndani na nje ya nchi, ndugu, marafiki, wakazi wa Lupaso na maeneo mengine walijitokeza kwa wingi kwa ajili ya kutoa heshima zao za mwisho kwa Rais Mkapa.

Mkapa alifariki dunia usiku wa kuamkia Julai 24, 2020 akiwa amelazwa hospitali kwa ajili ya matibabu jijini Dar es Salaam.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/29/ibada-ya-mazishi-ya-rais-mstaafu-mkapa-ikiendelea-watu-wafurika-kumuaga/

No comments:

Post a Comment