Monday, July 27, 2020

Membe asema Lissu amepata mapokezi makubwa awatumia ujumbe nzito CCM

Aliyekuwa waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amesema ameungana na mamilioni ya Watanzania kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu.

“Mapokezo makubwa na ya amani uliyoyapata leo kutoka kwa wananchi hasa Chadema ni ushindi wa upendo kwako,” aliandika Membe katika ukurasa wake wa Twitter.

Aliongezea kuwa “Salaam kwa watawala kuwa mitano inatosha! Sasa tujipange na tuunganishe nguvu tutashinda,”aliandika Membe.

Membe ambaye amejiunga na chama cha ACT-Wazalendo baada ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kumfuta uanachama.

Kiongozi huyo amechukua  fomu ya kugombea urais kupitia chama cha ACT-Wazalendo.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/28/membe-asema-lissu-amepata-mapokezi-makubwa-awatumia-ujumbe-nzito-ccm/

No comments:

Post a Comment