Maafisa hao pia waliipata bastola yake sakafuni, kando yake ikiwa na vifaa vya kusafishia bastola. Picha: Hisani
Kisa hicho kilifanyika Jumanne, Julai 28, 2020
Alikimbizwa kwa ndege hadi katika hospitali ya Medina alikothibitishwa kufariki
Afisa wa polisi wa utawala amejiua kwa kujifyatulia risasi katika kaunti ya Mandera alipokuwa akiisafisha bastola yake.
Katika kisa hicho kilichofanyika Jumanne, Julai 28, Evans Mwangi mwenye cheo cha coporal aliyekuwa akifanya kazi katika kituo kimoja cha kuundia sola alipatikana na maafisa wenza akiwa amelala sakafuni na jeraha la risasi bastola yake ikiwa kando.
Mwangi alisafirishwa hadi katika hospitali ya Medina alikothibitishwa kufariki.Picha: Hisani
‘’ Leo mwendo wa saa 2.30pm tukiwa katika kambi ya Raya SOG, polisi wa AP CPL Evans Mwangi alienda katika chumba chake kusafisha bastola yake aina ya Czeska, muda mfupi baadaye, tulisikia mlio wa risasi kutoka chumba hicho,’’ afisa mmoja alisema.
‘’Maafisa wenza walikimbia chumbani humo na kuupata mwili wa Evans sakafuni kichalichali huku akivuja damu nyingi kwenye paji la uso.’’ Aliongezea.
Maafisa hao pia waliipata bastola yake sakafuni, kando yake ikiwa na vifaa vya kusafishia bastola.
Mwangi alisafirishwa kwa ndege hadi katika hospitali ya Medina alikothibitishwa kufariki punde tu baada ya kuwasili.
Kisa hicho kinajiri siku chache tu baada ya afisa mwengine wa ngazi ya juu kumpiga risasi afisa mwenza na kumuua katika hali ya kutatanisha.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/29/polisi-ajifyatulia-risasi-kimakosa-na-kujiua-akisafisha-bunduki/
No comments:
Post a Comment