Monday, July 27, 2020

Lissu: Nilitamani nipige magoti niibusu ardhi nimeshindwa, mwili wangu una ramani ya makovu na vyuma vingi

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, amesema alitamani alivyoikanyaga ardi ya Tanzania apige magoti na kuibusu lakini ameshindwa kwa sababu goti halikunji.

Amesema katika utamaduni wa kawaida watu wanaoponea chupuchupu kama yeye huwa wakikanya udongo wa nchi yao wanapiga magoti na kubusu ardhi ya nchi yao.

“Nilitamani na mimi nifanye hivyo lakini goti halikunji, kwa hiyo siwezi tena kupiga magoti,” amesema Lissu.

Aidha, Lissu amesema jinsi alivyovaa unaweza usimuelewe kungekuwa na uwezekano wa kuvua magwanda hayo wote wangemkimbia kwa sababu mwili wake ukiacha kichwa na uso, mwili wake ni ramani za makovu ya risasi na visu vya madaktari.

“Huu mwili ni ramani za makovu ya risasi na visu vya madaktari, huu mwili una vyuma vingi,” amesema Lissu



source http://www.bongoleo.com/2020/07/27/lissu-nilitamani-nipige-magoti-niibusu-ardhi-nimeshindwa-mwili-wangu-una-ramani-ya-makovu-na-vyuma-vingi/

No comments:

Post a Comment