Viongozi wa Chadema wameondoka Ofisi za Makao Makuu kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), kumpokea Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa (Bara), Tundu Lissu, ambaye atatua uwanjani hapo saa 7.20 mchana huu.
Baada ya kupokelewa JNIA, Lissu ataelekea Ofisi za Makao Makuu ya Chadema, Mtaa wa Ufipa, jijini Dar es Salaam, ambako atazungumza na Waandishi wa Habari, wa vyombo vya kitaifa na kimataifa, mara baada ya kufika.
Mbali na viongozi wa Chadema wapi wafuasi wengine wa chama hicho wameahidi kwenda kumpokea Lissu.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/27/viongozi-wa-chadema-wamekwenda-kumpokea-lissu/
No comments:
Post a Comment