Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.
Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.
Zinazobamba ni pamoja na Mkapa Amzuia Membe, TAKUKURU Yawadaka 6 rushwa uchaguzi CCM na Waandamana kupnga alyeshinda kwa Wajumbe
Mkapa Azuia Membe kurejea nyumbani
Kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ametangaza kusitishwa kwa shughuli za kumpokea mtia nia wa kugombea wa urais wa chama hicho Bernard Membe mkoani Lindi kutoka na kifo cha Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Zitto ametangaza maamuzi hayo kupitia ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter leo Julai 25, 2020 na kusema chama hicho kinaendelea kutoa pole kwa familia ya Mkapa na taifa kwa ujumla.
Wagombea Viti maalum washikiriwa na TAKUKURU Rushwa kwa Wajumbe
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Mara inawashikilia watu 5 ambao ni wajumbe wa mkutano wa mkoa wa chama cha mapinduzi (CCM) kwa tuhuma za kupokea fedha kutoka kwa wagombea ubunge viti maalumu.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Mara, Alex Kuhanda amesema taasisi hiyo licha ya kukamata wajumbe hao pia imekamata kiasi cha Pesa Tsh. 3,300,000 ambazo zilikuwa tayari kupelekwa kwa wajumbe ili kuhujumu zoezi la kupiga kura.
Mshindi kura za maoni apingwa kwa maandamano
Ikiwa zimepitia siku kadhaa baada ya kunalizia kwa uchaguzi wa ngazi ya jimbo wa kupendekeza majina ya wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) watakaogombea ubunge na uwakilishi kwenye uchaguzi ujao mapema mwezi Oktoba.
Wakazi wa jimbo ka Magomeni visiwani Zanzibar wameandamana mpaka nyumbani kwa mshindi wa uchaguzi huo Jamal Kassim kwa lengo la kupinga ushindi wake baada ya uchaguzi uliofanywa na wa wajumbe chama.
Ukimalizia kusoma dondoo karibu tunagusia kwa kifupi njia za kuachana na mpenzi wako wa kwa amani
1. Kuwa na Uhakika na unachotaka kufanya: Kama huna uhakika juu ya hisia zako kwa mwenzi wako unapotaka kuvunja uhusiano bora usifanye hivyo maana utafanya moyo wako usiwe na maamuzi thabiti
2. Fikiria Sababu za Kuvunja Uhusiano: Unapojua sababu zinazopelekea wewe kuvunja mahusiano itakusaidia kutoa majibu ya uaminifu pale unapoulizwa
3. Maliza Mahusiano wewe Binafsi: Kama umekuwa na mpenzi wako kwa muda mrefu au kipindi chochote, uliwekeza muda na nguvu zako za kujenga mapenzi, hivyo ni busara mahusiano hayo ukayamaliza mwenyewe
4. Msikilize mwenzi wako: Hata kama umeshaamua na huwezi kubadili mawazo juu ya kuvunja mahusiano yenu, haina maana kuwa usimsikilize mwenzi wako
5. Kuwa Mtulivu na Makini: Unahitaji kuumaliza uhusiano na kuondoka mahali mlipo. Hata hivyo, ni busara kuwa mtaratibu na mpole
Je, nini uzoefu wako kuhusu kuacha au kuachwa katika mahusiano?
source http://www.bongoleo.com/2020/07/25/dondoo-za-leo-mkapa-amzuia-membe-takukuru-yawadaka-6-rushwa-uchaguzi-ccm-na-waandamana-kupnga-alyeshinda-kwa-wajumbe/
No comments:
Post a Comment