Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.
Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.
Zinazobamba leo ni pamoja na simulizi ya Lissu iliyosisimua, Mkewe kupewa na tuzo na mwisho ni juu ya wanasiasa Zanzibar kusikitika, kuna nini? Karibu;
SIMULIZI YA LISSU ILIVYOSISIMUA
TUNDU Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ametoa simulizi ya hali aliyonayo sasa iliyowafanya wasikilizaji kulengwa lengwa na machozi na simanzi zikitawala.
Lissu ametoa simulizi hiyo jana Jumatatu tarehe 27 Julai 2020 mbele ya viongozi wa Chadema, ndugu jamaa na marafiki katika Ofisi za chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam
Mwanasiasa huyo, alikuwa anazungumza akiwa ofisini hapo akitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam mara baada ya kuwasili akitoka nchini Ubelgiji.
Soma zaidi>>>
MKEWE APEWA TUZO
Nimeguswa kuandika hili, ukizingatia leo tunampokea Tundu lissu niliyempa jina la “Muujiza unaoishi”.
Natambua sana kuwa wanawake ni wavumilivu sana sana hasa kwenye shida ngumu wanazopitia. Lakini leo nitambue uwepo wa Mke wa tundu Lisu kama mpambanaji aliyekuwa beneti na mumewe wakati wote wa shida zilizomkuta Lisu.
Tumeona karibu miaka yote hii akiwa na mumewe beneti mpaka sasa tunaona Lisu anatembea akiwa mzima. HUU NI USHUHUDA MKUBWA sana.
Soma zaidi>>>
WANASIASA WASIKITIKA
VIONGOZI wa vyama vya siasa Zanzibar wameeleza kusikitishwa na kifo cha Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.
Viongozi hao wamesikitishwa wakimkumbuka Mkapa katika kuheshimu mfumo wa vyama vingi vya siasa, kuweka misingi imara na kuiweka Tanzania katika utulivu wa kisiasa.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Ada Tadea ambaye ni mgombea urais wa chama hicho, Juma Ali Khatib alisema Mkapa atakumbukwa kama rais wa kwanza Tanzania ya mfumo wa vyama vingi mwaka 1995 na kuweka misingi imara yenye kuzingatia usawa na demokrasia.
Soma zaidi>>>
Kumalizia dondoo hebu tuangalie jambo hili lililomkera mdau wetu juu ya watu kuwa na tabia ya kuwabusu watoto mdomoni.
Amesema, “Unakuta mtu kaja kutembelea mtoto wako au kamkuta umemshika anamchukua na kuanza kumpiga mabusu ya mdomoni. Huu ni uchafu sana mimi sipendi kabisa tabia hiyo”
Kimaadili tunaona haiko sawa sina hakika kama na wewe ungekipenda kitendo hicho.
Una maoni gani katika jambo hili?
source http://www.bongoleo.com/2020/07/28/dondoo-za-leo-simulizi-ya-lissu-iliyosisimua-mkewe-apewa-tuzo-na-wanasiasa-wasikitika/
No comments:
Post a Comment