Wednesday, July 29, 2020

Wanawake Wajawazito Waonywa Wakati wa Mazishi ya Mzee Mkapa

Weather or engine? Mkapa funeral riddle as delegation detours ...

Mwelekezi huyo alitoa onyo ya mapema kwa wanawake wajawazito. Picha: Hisani

Maelfu ya waombolezi walifika katika kijiji cha Lupaso kumpa heshima ya mwisho Mzee Mkapa

Viongozi mbali mbali, wakiwemo marais wastaafu waliongozwa na Rais Dkt Pombe Magufuli katika sherehe hiyo ya mazishi

Kulingana na itikadi za mazishi ya marais, wanajeshi hupiga mizinga 21 kama njia ya heshima kwa hayati

Wanawake wajawazito waliombwa kukaa pembeni wakati wa kupigwa mizinga hiyo ili kuepuka madhara yoyote

Sherehe ya mwisho ya safari ya aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu ya Jamuhuri ya Muunganao wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa ilikuwa ya ina yake, shughuli hiyo ikiongozwa na wanajeshi chini ya amri jeshi Rais John Pombe Magufuli.

Kulingana na mpangilio wa jeshi, kila kiongozi wa hadhi hiyo anapofariki, shughuli hiyo mzima husimamiwa na jeshi na kilele chake huwa mizinga 21 ya heshima ambayo hupigwa hewani na jeshi hilo punde tu baada ya kutiwa mashada ya maua kaburini.

Katika mazishi hayati Mkapa, mambo yalikuwa vivyo hivyo, mwelekezi wa sherehe hiyo akitoa onyo ya mapema kuhusu mizinga hiyo.

Kutokana na mshtuko wake, mwelekezi huyo alitoa onyo ya mapema kwa wanawake wajawazito akiwashauri kukaa pembeni wakati wa kupigwa mizinga hiyo.

Gun Salutes | The Royal Family

Shughuli hiyo mzima husimamiwa na jeshi na kilele chake huwa mizinga 21. Picha: Hisani

‘’Tukimaliza kuweka mashada ya maua, tunawaomba wanawake wajawazito kusonga pembeni ili kuzuia madhara yoyote.’’ alisema

Kando na wajawazito, aliwaomba wenye magari kufungua madirisha ya magari yao, waoga kukaa kando na pia kuwasihi waombolezaji wote wafungue midomo bila kuziba masikio.

Si hayo tu, aliwaomba majirani kuyafungua madirisha ya majengo yao ili kuzua uharibifu wowote.

Mzee Mkapa alifariki Ijumaa, Julai 24 akiwa na umri wa miaka 81 viongozi wa nchi mbali mbali wakimsifia kwa hatua alizopigisha Tanzania na Afrika kwa Jumla.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/29/wanawake-wajawazito-waonywa-wakati-ya-mazishi-ya-mzee-mkapa/

No comments:

Post a Comment