Tuesday, July 28, 2020

Breaking News: Rais magufuli atangaza rasmi uwanja Taifa uitwe Mkapa Stadium

 

Rais John Magufuli ametangaza rasmi Uwanja wa Taifa sasa utaitwa Uwanja wa Benjamin William Mkapa (Benjamin William Mkapa Stadium) kwa kuenzi mchango wake kwenye kuendeleza michezo.

Rais Magufuli ametoa wito huo kwenye shughuli ya kitaifa ya kuaga mwili wa Rais msaafu Benjamini mkapa aliyefariki usiku wa kumkia Julai 24,2020 jijini  Dar es salaam.

“Mzee Mkapa aliujenga uwanja mkubwa wa michezo,kwa sasa wengi wanataka uwanja uitwe ‘Mkapa Stadium’, Mzee Mkapa alikuwa hapendi vitu viitwe kwa jina lake, lakini kwakuwa hawezi kuniadhibu chochote amelala hapo, natamka rasmi uwanja ule uitwe Mkapa Stadium” amesema Rais Magufuli



source http://www.bongoleo.com/2020/07/28/breaking-news-rais-magufuli-atangaza-rasmi-uwanja-taifa-uitwe-mkapa-stadium/

No comments:

Post a Comment