Monday, July 27, 2020

TFF imesema wanamchukulia hatua kali kocha wa Yanga

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema litamchukulia hatua za kinidhamu kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael kwa kumfikisha katika vyombo husika kutokana na matamshi ya kibaguzi aliyoyatoa kwa mashabiki wa timu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo imeeleza kuwa TFF itawasilisha taarifa za Luc Eymael, kwa shirikisho la kimataifa la mpira wa Miguu (FIFA) kuhusu kauli za kibaguzi ili wachukue hatua kwa vile kocha huyo anaweza vitendo hivyo katika nchi nyingine.

Mwaka jana FIFA ilifanya marekebisho ya kanuni zake za nidhamu na kuongeza adhabu kwa wanaofanya vitendo vya kibaguzi kwa vile ni ukiukwaji mkubwa wa haki za msingi wa za binadamu.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/27/tff-imesema-wanamchukulia-hatua-kali-kocha-wa-yanga/

No comments:

Post a Comment