Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema maandalizi ya kusafirisha mwili wa Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa kutoka jijini Dar es salaam mpaka mkoani Mtwara yemekamilika kwa asilimia mia moja.
Akizungumza dakika chache baada ya kufika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam inapofanyika tukio la kuaga mwili wa Rais huyo Waziri Majaliwa amesema shughuli ya kitaifa hapo kesho itaanza mapema saa 4 asubuhi.
“Misaa ya wafu itafanyika majira ya saa 12 asubuhi na milango ya uwanja wa uhuru hapa itafunguliwa asubuhi baada tu ya misa tuanza shughuli ya kitaifa ya kuaga na baada ya kumaliza kuaga kwa viongozi wa kitaifa tutasafirisha mwili kwa ajili ya mazishi mkoani Mtwara” amesema Waziri Majaliwa.
Aidha Waziri ameongeza kuwa wananchi wa kawaida watamaliza shughuli ya kuaga leo kwakua kesho ni zamu ya viongozi tu hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi leo kumuaga rais huyo mstaafu.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/27/waziri-mkuu-maandalizi-shughuli-kumuaga-mzee-mkapa-yamekamilika/
No comments:
Post a Comment