Wawili hao walikuwa na mzozo wa muda tangu walipofanya harusi
Jama huyo alikuwa akimshuku mkewe kuwa na mahusiano mengine nje ya ndoa
Wakizozana na mke huyo eneo la Gilgil, jamaa huyo alimdunga kisu na kumuua akajisalimisha kwa polisi baada ya kubugia sumu
Mwanamme mwenye umri wa miaka 34 amemuua mkewe kwa kumdunga kisu mara kadhaa na kisha kunywa sumu na kujisalimisha kwa polisi.
Kulingana na kisa hicho kilichochapishwa katika jarida la Nation, kamanda wa polisi eneo la Gilgil John Onditi alieleza kuwa jamaa huyo alifanya unyama huo kufuatia mzozo wa kifamilia.
‘’ Alijisalimisha baada ya kugundua kuwa polisi ilisambaza nambari ya usajili ya gari lake kila mahali,’’ Onditi alisema.
Baada ya kujisalimisha, bwana huyo alianza kuugua ghafla na kutapika alipokuwa akihojiwa na polisi. Alikimbizwa hospitalini kulikothibitishwa kuwa alikuwa amekunywa sumu.
Atafikishwa kortini kushtakiwa kwa kosa la mauaji . Picha: Hisani.
‘’ Tuliweza kupata chupa iliyokuwa na sumu hiyo kwenye gari lake. Anaendelea kupata afueni hospitalini chini ya ulinzi mkali wa polisi,’’ aliongezea kamanda huyo.
Jamaa huyo atafikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kosa la mauaji punde tu atakapokuwa imara kiafya .
Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kusubiri upasuaji kubaini chanzo ha kifo.
Visa vya mizozo kati ya wanandoa vimezidi kupanda, utafiti ukibaini kuwa umakini ndio chanzo kuu.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/29/mume-amuua-mkewe-akunywa-sumu-na-kujisalimisha-kwa-polisi/
No comments:
Post a Comment