Msanii Diamond alitangaza kuwa atafunga pingu za maisha akiadhimisha umri wa miaka 31 Disemba
Jihandi Mark anadaiwa kuwa mrembo aliyepata bahati kutiwa pete na msanii huyo
Hayawi hayawi huwa na yakisemya yapo kama hayapo yaja, hatimaye habari kuhusu mrembo aliyebahatika kupata penzi kamili ya msanii maarufu wa Bongo Diamond Platnamz amebainika.
Jihandi Mark mwanamtindo tajika ambaye pia ni mwanabiashara ndiye anayedaiwa kuwa katika kiini cha moyo wa Diamond, mipango ya harusi ikianza rasmi chini chini.
Inadaiwa kuwa msanii Mondi alianza uhusiano na Jihandi Mark miezi michache tu baada ya kumtema mrembo wa Kenya ambaye pia alikuwa msanii mwenza Tanasha Donna.
Penye moshi pana moto, uvumi umeenea kuwa Diamond tayari ameanza maandalizi ya kumfungisha rasmi mrembo huyo pingu za maisha. Kulingana na mdaku wetu, sherehe ya harusi kati ya wawili hao itaandaliwa faraghani.
Wiki moja tu iliyopita Mama Dangote alithibitisha uhusiano wa Jihandi na msanii Mondi baada ya kuichapisha picha ya mrembo huyo mtandaoni huku akimrundia sifa si haba.
Haya ni baada ya mrembo huyo kuhudhuria hafla iliyoandaliwa na lebo Wasafi kumsherekea Zuchu kwa hatua kubwa aliyopiga katika fani ya usanii tangu kujiunga na lebo ya Wasafi.
Nani asiyejua kuwa Mama Dangote akitia sahihi mwanadada naye Mondi ni kutii na kumkwachua? Basi ndivyo mambo yalivyo, letu ni kusubiri miwani machoni.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/28/diamond-aanza-mipango-ya-harusi-bibi-harusi-ajulikana-kisirisiri-uhondo-kamili/
No comments:
Post a Comment