Mwanamke aliyefungwa na mumewe kwa nyororo nguzoni kwa zaidi saa 10 hatimaye ameokolewa. Picha: Hisani
Uche alimfunga mkewe kwenye nguzo ya nyumba kwa kutumia nyororo na kufuli
Alitoweka na ufunguo asionekana tena
Majirani walieleza kuwa alimpiga mwanawe kichwa kwa nyororo hiyo alipomzuia asimfanyie mamake unyama huo
Ngozi Chukwani, mwanamke aliyefungwa na mumewe kwa nyororo nguzoni kwa zaidi saa 10 hatimaye ameokolewa.
Mume huyo aliyetambuliwa kama Uche alitoweka na ufunguo baada ya kumpiga na kumtia nyororo na kumfunga kwa kufuli mkewe.
Kulingana na kisa hicho kilichochapishwa katika jarida la Tribune, Uche alimpiga kichwa mwanawe wa kike aliyejaribu kumzuia asimfunge na kumpiga mamake.
Nchekwube Saints Anakor, naibu gavana wa usalama eneo hilo alilaani vikali kitendo hicho.
Alimuamuru fundi mmoja wa vyuma kumfungua mama huyo huku akiahidi kumchukulia bwana huyo hatua za kisheria kwa kumfanyia mama huo unyama.
Majirani walieleza kuwa wawili hao walikuwa na mizozo ya kila mara na kuwa bwana huyo alikuwa na mazoea ya kumpiga mkewe mbele ya watoto. Haibaniki ni nini kilimpelekea jamaa huyo kumfunga mkewe siku ya kisa na kutoweka.
Kisa hicho kilifanyika katika jimbo la Eboni, Nigeria Jumatano, Julai 29 wengi wakishangaa ni kwanini mume huyo aliamua kuchukua hatua hiyo.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/30/kisa-cha-mume-aliyempiga-kufuli-mkewe-kwa-nyororo-ukutani-na-kutoweka-na-ufunguo/
No comments:
Post a Comment