Friday, July 24, 2020

Makonda: Mimi ni mmoja wa vijana tulionufaika ya Rais Mstaafu Mkapa

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema yeye ni miongoni mwa vijana walionufaika na maisha ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.

Makonda aliandika ujumbe huo leo katika ukurasa wake wa twitter kuwa Rais Mstaafu Mkapa apumzike kwa amani na kwamba alipanda mbegu njema maishani mwake.

“Mimi ni mmoja wa vijana tulionufaika na maisha yako hapo duniani, pumzika kwa amani huku ukitambua ulipanda mbegu njema maishani mwangu. REST IN  ENTERNAL PEACE BABA,” aliandika Makonda

Rais Mstaafu Mkapa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa amelazwa hospitali kwa ajili ya matibabu jijini Dar es Salaam.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/24/makonda-mimi-ni-mmoja-wa-vijana-tulionufaika-ya-rais-mstaafu-mkapa/

No comments:

Post a Comment