Wednesday, July 29, 2020

Mzee wa Miaka 70 Ashirikiana na Mwanawe Kumnajisi Mjukuu

James Kayata Muia (L) and his son, Benjamin Mutinda Muia (R), are accused of defiling their 11-year-old female relative. [PHOTO: PATRICK MUTISYA | K24 DIGITAL]

Iwapo watapatikana na hatia, watatumikia kifungo cha miaka 20 kulingana na sheria. Picha: Hisani

Wawili hao walikamatwa Machakos Jumanne, Julai 28

Mwanafunzi huyo alieleza kuwa babu yake alianza kumtendea unyama huo tangu 2016

Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 70 pamoja na mwanawe wa miaka 28 wamejipata pabaya baada ya unyama waliokuwa wakimtendea msichana mdogo aliyekuwa akiishi nao kubainika.

Kulingana na kisa hicho kilichochapishwa katika jarida la K24, James Kayata Muia na mwanawe  Benjamin Mutinda Muia wamekuwa wakimnajisi mwanafunzi wa miaka 15 tangu 2016 hadi 2020.

Msichana huyo ambaye alikuwa katika darasa la tano ni mjuukuu wa Benjamin.

Akihojiwa na polisi, mwanafunzi huyo alieleza kuwa Mutinda ambaye ni mjomba wake alianza kumtendea unyama huo tangu 2016.

‘’ Mwaka huo, Mutinda alininajisi mara moja. Tangu 2017, alikuwa anafanya kila anapotaka. Kila baada ya kitendo hicho, alikuwa akinionya dhidi ya kumwambia yeyote kuhusu kisa hicho,’’ Msichana huyo alieleza.

Alieleza kuwa babu yake alianza kumfanyia kitendo hicho 2020.

‘’Hivi majuzi aliniita kwa nyumba yake akaniuliza; ‘ umewahi kuvunjwa ubikira?  Nilimuuliza: unamaanisha nini? Alijibu kwa kusema, njoo katika chumba changu cha kulala nikuonyeshe ninachomaanisha. Nilikuwa na dadangu mkubwa. Alimtuma dukani kununua pipi kabla kuniita chumbani na kunibaka kwa siku tatu,’’ Msichana huyo alisimulia.

Wazazi wa mtoto huyo ambao hawakuwa wakiishi kijiini waligundua kuwa mwanao hakutaka kuishi na kina babu tena, alipoulizwa, mtoto huyo alisimulia kuhusu unyama aliotendewa muda huo wote.

Walimpeleka katika hospitali ya rufaa ya Kathiani Jumanne kuchunguzwa na madaktari huku babu huyo na mwanawe wakikamatwa na polisi.

‘’Tunasubiri kupata ripoti ya polisi kabla kuwafungulia mashtaka wawili hao tunaowazulilia katika kituo cha polisi cha Kathiani,’’ Naibu OCP John Kimathi alisema.

Iwapo watapatikana na hatia, watatumikia kifungo cha miaka 20 kulingana na sheria.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/29/mzee-wa-miaka-70-ashirikiana-na-mwanawe-kumnajisi-mjukuu/

No comments:

Post a Comment