Wednesday, July 22, 2020

Zitto Aitabiria CCM Ushindi Mkubwa Oktoba

Majukumu ya ACT Wazalendo: Yamnyima Urais Zitto Kabwe - Bongo5.comKiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe amesema kuna uwezekano mkubwa bunge lijalo likatawaliwa zaidi na wawakilishi kutoka chama kimoja cha CCM kutokana na kuona uwezekano mkubwa wa uchaguzi huo kutumia nguvu kubwa za dola.

Zitto amesema hayo wakati akijibu swali aliloulizwa na mwanahabari mkongwe nchini Jenerali Ulimwengu wakati wa mahojiano maalum aliyofanya akiwa nyumbanii kwake Masaki Jijini Dar es salaam.

“Tunaingia kwenye uchaguzi huu tukiwa na mambo mawili kichwani moja ni kuna uwezekano mkubwa wa uwakilishi baada ya oktoba kutoka chama kimoja au pili kama tutafanikiwa kulinda demokrasi itayasaidia kuunda serikali yenye sera nzuri za kidemorasia ya vyama vingi, mimi naona utakuwa uchgazi unaotumia nguvu kubwa ya dola” amesema Zitto.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/22/zitto-aitabiria-ccm-ushindi-mkubwa-oktoba/

No comments:

Post a Comment