Wednesday, July 22, 2020

Yanga Yaendelea Kudondosha Pointi Muhimu

Klabu ya Yanga bado inaendelea kudondosha pointi muhimu katika vita ya kugombani nafasi ya pili dhidi ya matajili wa Dar es salaam Azam Fc baada ya kubanwa na Mtibwa Sugar kwa sare ya goli 1-1 kwenye mchezo wa 37 wa ligi kuu bara.

Yanga ambayo ilikuwa ya kwanza kuruhusu goli kwenye dakika ya 28 kupitia kwa Winga wa Mtibwa Haruna Chanongo baada ya makosa ya mabeki wa kati wa Yanga.

Yanga ilisawazisha mnamo dakika ya 85 kupitia kwa beki wa kulia Adeyum Saleh baada ya sare ya elo yanga inasalia nafasi ya pili ikiwa na jumla pointi 69 pointi moja tatu mbele ya Azam wenye pointi 66 na mchezo mmpja mkononi.

Mchezo wa mwisho wa Yanga utapingwa mnao Julai 27 ,2020 kwenye dimba la Samora dhidi ya wanapaluengo Lipuli Fc wanaoshika nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi kuu bara inayotarajia kukamilika siku hiyo.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/22/yanga-yaendelea-kudondosha-pointi-muhimu/

No comments:

Post a Comment