Wednesday, July 22, 2020

Vijana 3 Waua Marafiki 2 Kufuatia Mzozo wa Mchezo wa Kamari

Witch doctor arrested for impregnating 02 sisters aged 16 & 18 ...John Wanjiru, Samuel Wachira Ngatia na Dennis Makori Nyakundi. Walizuiliwa katika kituo cha polisi baada ya kuwaua marafiki zao

Watano hao walikuwa wakizozana katika duka moja la kufanya mchezo wa Kamari baada ya kushiriki mchezo huo pamoja

Waliwapiga wawili hao kwa mawe hadi kifo

Mchezo wa Kamari umekuwa maarufu sana haswa kati ya vijana, hii ni kokana na ushabiki mkubwa wa mpira wa kandanda.

Kampuni za Kamari huweki donge nono za ushindaniwa kama njia safi ya kuwavutia wenye tamaa ya pesa.

Huku baadhi wakijishindia hela hizo, wengi husalia kwa masikitiko huku macho yakifunguka baada ya hela zao kuliwa na hatimaye kufanya madhambi kiasi cha kujiua.

Vijana watano waliokuwa marafiki wa karibu kabla na wakati wa kushiriki mchezo huo wa Kamari sasa wamekuwa maadui wakubwa, wawili wao wakiuliwa baada ya kutofautiana katika mchezo huo.

John Wanjiru, Samuel Wachira Ngatia na Dennis Makori Nyakundi walinaswa na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Kayole baada ya kuwaua marafiki wao wawili.

Kulingana na taarifa ya polisi, Watatu hao walijibizana na wenzao katika duka moja la Kamari katika mtaa wa Kayole kabla kushikwa na hasira na kuwaua kwa mawe.

Covid-19: Police arrest worshippers in Nyandarua church - Daily Nation

Watatu hao watasalia kuzuizini kwa siku 10 zaidi, hii ni baada ya polisi kupewa ruksa kuwazuia huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo.

Aidha, hakimu mkuu wa mahakama ya Makdara ameagiza kufanyika upasuaji wa miili hiyo na vile vile watatu hao kufanyiwa uchunguzi wa akili kabla kufika mbele yake kujibu mashtaka ya mauaji siku 10 baadaye.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/22/vijana-3-waua-marafiki-2-kufuatia-mzozo-wa-mchezo-wa-kamari/

No comments:

Post a Comment