Wednesday, July 22, 2020

Mbunge Aliyetaka Diamond Awekewe Sanamu Apingwa Chini Kura Za Maoni

HabarileoUnakumbuka wakati wa bunge la 11 Mei 31, 2016 mbunge mmoja alisimama bungeni na kutoa hoja kuwa sanamu ya askari katikati  ya jiji la Dar es salaam itolewe na kuweka ya msanii Diamond Platnumz kutokana na kujituma kwake kwenye tasni ya muziki nchini.

Mbunge huyo alikuwa Goodluck Mlinga aliyepeperusha bendera ya chama cha mpinduzi (CCM) kwenye jimbo la Ulanga mkoani Morogoro na alikuwa mmoja kati ya wagombea kadhaa walijitokeza kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge jimboni hapo.

Matokeo ya mwisho ya aliyepitishwa jimboni humo alikuwa mwanaCCM Salmu Hashimu ambaye ajizolea kura 219 huku Goodluck Mlinga akishika nafasi ya pili kwa kupata kura 123 huku nafasi ya tatu ikishikwa na Fadhili Lilongeli aliyepata kura 114.

Mlinga alijzolea umaarufu kwenye bunge la 11 kutoka na hoja zake mbali na kutaka diamond awekewe sanamu pia aliwahi kutoa hoja ya kutaka Tanzania ianze kuuza bangi kama zao la biashara kwa nchi ambazo zimehararisha matumizi ya bangi.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/22/mbunge-aliyetaka-diamond-awekewe-sanamu-apingwa-chini-kura-za-maoni/

No comments:

Post a Comment