Tuesday, July 21, 2020

Watoto Wa Nyerere Waangukia Pua Ubunge Butiama

Huwezi Amini Watoto wa Nyerere Wapigwa Chini Vibaya Kura za Maoni ...Mchakato wa kuchagua wagombea wa ubunge ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) unaendelea kote nchini katika ngazi ya awali kwenye majimbo husika kwa makada wa chama hicho waliotiania kuomba kuchaguliwa na wajumbe wa mkutano wa majimbo.

Katika Jimbo la Butiama watoto wawili wa baba wa Taifa Mwalimu Jullius Nyerere walijitosa kugombea kwenye jimbo hilo lilikuwa linaongozwa na mbunge aliyemaliza muda wake Nimrod Mkono.

Watoto hao wa baba wa taifa wameangukia pua baada ya  Makongoro Nyerere kupata kura 5 huku nduguye  Madaraka Nyerere akijizolea kura 2 kwenye mchakato huo ambapo mshindi alikuwa Jumanne Sagini aliyejizolea jumla ya kura 84 akifuatiwa na Frank Mahemba aliyepata kura 80.

Ikumbukwe kuwa mchakato wa awali wa ndani ya chama umeanza jana Julai 20,2020 na utaendelea kwa siku kadhaa kabla ya ngazi za juu za Wilaya na taifa kukaa na kuchagua jina moja.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/21/watoto-wa-nyerere-waangukia-pua-ubunge-butiama/

No comments:

Post a Comment