Tuesday, July 21, 2020

Mwalimu Auza Mafahali wa Shule, Ajilipa Mshahara wa Miezi Sita

Zambia Beefmaster bulls and Bonsmara bulls available for sale ...

Mbagaya  aliwauza mafahali watatu na kujilipa mshahara wa miezi sita. Picha; Hisani

Mbagaya aliamua kuwanadi mafahali hao baada ya bodi ya shule hiyo kudinda kumlipa tangu Mei

Mwalimu huyo wa somo la biashara alieleza kuwa aliwauza mafahali hao kwa TSh 1,650,000 na kujilipa mshahara wa miezi sita

Mwalimu huyo aliishukuru bodi ya shule hiyo kwa kumpa nafasi ya kufunza humo

Philip Mbagaya, mwalimu wa somo la biashara katika shule ya upili ya Indangalasia, kaunti ya kakamega amewaacha wengi vinywa wazi kwa njia aliyotumia kujilipa mshahara wa donge nono.

Mbagaya ambaye aliajiriwa na bodi ya shule hiyo aliwauza mafahali watatu na kujilipa mshahara wa miezi sita baada ya kudai kuwa bodi ya shule hiyo ilidinda kumlipa.

Mwalimu huyo alisisitiza kuwa hakuwa na lolote lingine la kufanya haswa baada ya mwalimu mkuu wa shule hiyo kudinda kupokea simu zake.

‘’ Sijalipwa tangu mwezi Mei.  Familia yangu inanitegemea na bodi ya shule inaniambia sitalipwa hadi pale shule zitakapofunguliwa,’’ Mwalimu huyo alinukuliwa na jarida la Nation.

Cattle

Mbagaya alieleza kuwa aliwauza mafahali hao kwa TSh 1,650,000 na kuweza kuilipa mshahara wa miezi sita. Aidha alichukua nafasi hiyo kuishukuru bodi kwa kumpa nafasi ya kufunza katika shule hiyo.

‘’  Nimejilipa hadi Disemba, naushukuru usimamizi wa shule kwa kunipa nafasi katika shule hiyo. Nawatakia heri wakati huu mgumu.’’ Aliongezea.

Kando na hivyo, mwalimu huyo aliimba wizara ya elimu kubuni sheria itakayohakikisha kuwa walimu walioajiriwa na bodi wanapata mishahara yao hadi 2021 shule zitakapofunguliwa tena.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/21/mwalimu-auza-mafahali-wa-shule-ajilipa-mshahara-wa-miezi-sita/

No comments:

Post a Comment