Tuesday, July 21, 2020

Gwajima Ahaidi Kumtoa Mdee Asubuhi Tu

ImageMtiania wa ubunge jimbo la Kawe na askofu wa kanisa la Ufufuo na uzima Josephat Gwajima amehaidi kulirudisha jimbo la Kawe ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) mapema tu asubuhi baada ya mchakato wa kupiga kura kumalizika Oktoba 28, 2020.

Gwajima akizungumza alipopewa kwenye nafasi ya dakika moja kujinadi mbele ya wajumbe wa jimbo la Kawe kwenye mchakato wa awali wa kuomba kura kabla ya zoezi zima kuanza mapema hapo baadae.

“Chagua Josephat Gwajima, huyu ndiyo mtu pekee atakayekurudishia jimbo lako, asubuhi na mapema tumeshawachinjia shingoni” amesema Gwajima.

Jimbo la kawe kwa kipindi cha miaka kumi na tano (15) limekuwa likiongozwa na mbunge wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Halima Mdee aliyemaliza muda wake baada ya kuvunjwa kwa bunge la 11.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/21/gwajima-ahaidi-kumtoa-mdee-asubuhi-tu/

No comments:

Post a Comment