Wednesday, July 22, 2020

Kabeji ni Kiungo Muhimu Katika Kuzuia Covid19 – Utafiti

Cabbage-farm

Kabeji huukinga mwili dhidi ya virusi vya corona. Picha: Hisani

Ripoti za mapema zimebaini kuwa ulaji wa mboga ya kabeji una umuhimu mkubwa katika kupambana na kuzuia virusi hatari vya corona, haya ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa Uropa.

Utafiti huo umebaini kuwa kabeji ama tango zinapoliwa kwa wingi haswa gramu moja zaidi kila siku hupunguza kiwango cha vifo hadi 13.6% na 15.7 mtawalia.

Kulingana na ripoti ya jarida la South China Morning Post, utafiti huo ulofanyika uropa umebaini  kuwa kabeji inapoliwa kwa kila njia, mbichi, ikipikwa ama hata inapochanganywa na tango, husaidia pakuwa katika kujenga kinga dhidi ya virusi hatari vya corona.

Utafiti huo ambao hadi sasa haujaidhinishwa na shirika la afya ulimwenguni WHO, ulifanyiwa Uropa na kuonyesha jinsi kabeji ilivyo na uwezo mkubwa wa kuzuia virusi vinavyoambukiza corona.

11 Best Cabbage Recipes | Patta Gobhi Recipes - NDTV Food

Kulingana na aliyekuwa mwenyekiti wa  ushirikiano wa WHO kuhusiana na magonjwa hatari ya pumu Dr. Jean Bousquet, lishe ni muhimu zaidi na haiwezi kupuuza kama njia mojawapo ya kuapambana na virusi hatari vya corona.

Iwapo utafiti huo utadhibitishwa na kupewa muhuri, basi kabeji itakuwa nadra maana kila nchi itakuwa mbioni kuikimbilia kama njia ya kujikinga.

Virusi vya corona vimekuwa donda dungu, watafiti sasa wakieleza kuwa wapo katika awamu ya mwisho kuhusu kufanya majaribio ya  chanjo na tiba kwavyo.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/22/kabeji-ni-kiungo-muhimu-katika-kuzuia-covid19-utafiti/

No comments:

Post a Comment