Tuesday, July 21, 2020

Tundu Lissu Kutua Dar Mchana Kweupe

Interview with Tundu Lissu, opposition leader, Tanzania - YouTubeMakamu  mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesisitiza kuwa ifikapo Jumatatu ya Julai 27, 2020 saa 7:20 atarejea nchini akitokea nchini Ubeligiji alikokuwa akipatiwa matibabu.

Akizungumza kwenye hotuba aliyotoa leo kwa njia ya mtandao wa Youtube, Lissu amesema atarudi nyumbani ili hali anajua kabisa hali ya usalama wake sio swali kama alivyoondoka.

“Baada ya miaka mitatu ya matibabu wakati wa kurejea nyumbani umewadia na ifikapo tarehe 27,Julai nitakanyanga ardhi ya nyumbani Tanzania kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitatu majira ya saa 7:20 kwenye uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es salaam”amesema Lissu.

Aidha Lissu amesema mwenyekiti wa chama hicho  Freeman Mbowe ameandika barua ya kuomba ulinzi kwa wakuu wa vyombo vya usalama nchini  lakini mpaka sasa hawajapata majibu yoyote ya kuhusu kuhakikishiwa usalama wake anapowasili nchini.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/21/tundu-lissu-kutua-dar-mchana-kweupe/

No comments:

Post a Comment