Tuesday, July 21, 2020

Tundu Lissu kurudi nchini Jumatatu, awatumia salamu waliotaka kumuua

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, amesema ataingia nchini Jumatatu ya Julai 27, 2020 majira ya saa 7:20 mchana  akiwa kwenye ndege ya Shirika la Ethiopia.

Lissu ameyasema hayo leo wakati akizungumza na Watanzania kuhusiana na safari yake ya kurejea nchini.

“Kwa kipindi hiki nina mambo mengi sana yaliyo kichwani mwangu ambayo ni vigumu kuyaeleza yote naomba nisema tu wale waliotumwa kuja kuniua na waliowatuma hawakutegemea kwamba siku kama ya leo nitakuwepo na nitakuwa nazungumza nyumbani,” amesema Lissu

Lissu anarejea nchini baada ya kuondoka kwa miaka mitatu kutokana na kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 na kusafirishwa nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/21/tundu-lissu-kurudi-nchini-jumatatu-awatumia-salamu-waliotaka-kumuua/

No comments:

Post a Comment