Tuesday, July 21, 2020

Sugu awapiga vijembe waliotimkia CCM na kupigwa chini kwenye kura za maoni

Aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu amewarushia kijembe waliokwenda kuunga juhudu  na kupigwa kwenye kura za maoni.

Sugu aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa twitter huku akisema licha ya matuso yote waliyotukana waunga mkono lakini bado Chama cha Mapinduzi (CCM) hakijawakubali.

“Pamoja na matusi yoooote waliotukana waunga mkono juhudi lakini bado CCM hawaja-appreciate, bado wamewapiga chini kwenye maoni wallah,” alindika Sugu.

Baadhi ya wabunge waliokuwa Chadema baada ya kuhamia CCM kwa kudai wanaunga mkono juhudi za serikali iliyopo madarakani wamepigwa chini kwenye uchaguzi wa kura za maoni.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/21/sugu-awapiga-vijembe-waliotimkia-ccm-na-kupigwa-chini-kwenye-kura-za-maoni/

No comments:

Post a Comment